MSAGA SUMU : MWANAUME MASHINE SIO MATUSI MAANAYAKE NI HII HAPA
Msanii wa muziki wa Singeli Bongo, Msaga Sume amefunguka mafanikio ya ngoma hiyo tangu ilipotoka.
Ngoma hiyo ambayo ilitoka May 12 mwaka huu imekuwa na mwiitikio mkubwa mtaani kutokana na ujumbe wake. Akizungumza na FNL ya EATV Msaga Sumu amesema ngoma hiyo imekuwa na mafanikio makubwa ila mashabiki wamekuwa na tafsiri ambayo siyo.
“Mashabiki walivyopokea wamepokea kitofauti ndio sababu ya kupendwa, mashabiki wamepokea kama nimeenda kinyume fulani, wanavyoona kama nimeleta matusi fulani ndio maana ilipokelewa kwa ghafla na haraka,” amesema.
“Sisi watu wa uswahilini tuna maneno yetu na nilijua nikitoa nyimbo hii watu wengi watajua nimeenda kinyume lakini kumbe mimi nipo sahihi,” ameongeza.
Hata hivyo ameeleza kitu alichokusudia katika ngoma hiyo na kuongeza kuwa imekuwa ikipendwa na watu wote hata wa rika ya chini kabisa.
“Mwanaume ni mpiganaji, mtafutaji, muangaikaji, mwanaume hakatii tamaa, katika maisha mtu kama mimi nimepitia vitu vingi sana nikaona ngoja niweke kitu kama mwanaume mashine lakini nikaweka mafumbo fulani,” amesema Msaga Sumu.
No comments