MSIGWA AWAAMBIA POLISI HAWAWEZI KUMPANGIA CHA KUSEMA
Anatakiwa kuripoti kwa RCO asubuhi
Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa amesema polisi hawawezi kumpangia nini cha kusema na wala sio majukumu yao.
“Wamenikamata nikitimiza majukumu yangu ya kibunge! Sitanyamaza,” ameandika Mchungaji Msigwa katika ukurasa wake wa Twitter.
Msigwa aliachiwa huru jana usikukwa dhamana baada ya kukamatwa akiwa kwenye mkutano wa hadhara.
Msigwa ameachiwabaada ya kudhaminiwa na wadhamini wawili Alex Kimbe pamoja na Mwenyekiti wa Bavicha, Iringa Leonce Marto.
Msigwa alishushwa jukwaani kwa nguvu akiwa anahutubia mkutano wa hadhara katika Kata ya Mlandege Manispaa ya Iringa na anatuhumiwa kwa kosa la uchochezi dhidi ya vyombo vya usalama .
Marto amesema mikutano yake imefungiwa na hapaswi kuendelea na ziara yake katika kata nyingine mpaka hapo OCD atakapo amua vinginevyo.
Leo Mbunge anatakiwa kuripoti kwa RCO na huenda kesi ya uchochezi ambayo tayari imeshafunguliwa jalada lake ikapelekwa mahakamani .
Amesema Mbunge huyo atazungumza na vyombo vya habari leo mchana kuweka wazi madhila yaliyompata wakati akitekeleza wajibu wake kwa wananchi.
No comments