Breaking News

Waziri Mkuu Atoa Ujumbe Mzito Kwa Wabunge


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka wabunge kuonyesha mshikamano na kupendana ili waendeleze jukumu la kuishauri Serikali.

Kiongozi huyo wa Serikali alitoa kauli hiyo jana  katika futari aliyoiandaa kwa wabunge iliyofanyika katika viwanja vya Bunge.

“Nasisitiza mshikamano miongoni mwetu katika Bunge hili la Bajeti tangu lianze, tumeonyesha mshikamano na tuendeleze mshikamano huu na kupendana miongoni mwetu ili tuendelee na jukumu la kuishauri serikali,” alisema Majaliwa.

Naye Spika wa Bunge, Job Ndugai akitoa shukrani kwa niaba ya wabunge alisema ni heshima kubwa kwani kualikwa na Waziri Mkuu si jambo ndogo.

“Kwa hiyo tujihesabie katika waliobahatika. Mheshimiwa Waziri Mkuu, tunakushukuru na tunakuombea Mwenyezi Mungu akuongezee pale palipopungua,” alisema Spika Ndugai.

Futari hiyo iliyoandaliwa na Waziri Mkuu, imehudhuriwa na wabunge karibu wote wakiwamo wa upinzani.

No comments