Breaking News

Msuva amerudi Tanzania na mambo 12 toka Morocco

Mcheezaji wa kimataifa wa Tanzania anaechezea klabu ya Difaa El Jadid ya Morocco amewasili nchini leo August 31, 2017 kwa ajili ya kuungana na wachezaji wengine kwenye kambi ya Taifa Stars kujiandaa na mchezo wa kirafiki wa kalenda ya FIFA dhidi ya Botswana September 2, 2017 uwanja wa Uhuru, Dar.

Shaffihdauda.co.tz ilikuwepo uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl. Julius K. Nyerere na kufanikiwa kupiga story na Msuva ambapo amejibu maswali mengi kuhusu maisha yake mapya nchini Morocco.

Tofauti ya Tanzania na Morocco upande wa soka

Nimefika kule nimepokelewa vizuri na nimeweza kufanya kitu ambacho wao wenyewe wameona nafaa kuwa pale kwa hiyo naona hakuna tofauti sana na Tanzania.

Kuhusu kubadilishwa position ya uchezaji

Kaika maisha chochote unachopewa unatakiwa kupokea, kama sisi wacheza mpira mwalimu anaweza akakuangalia akaona huyu anafaa kucheza namba mbili, naweza kwenda nchi nyingine mwalimu akaniangalia akaona naweza kucheza nafasi nyingine kulingana na mfumo wake.

Kwa hiyo sishangai hapa nilikuwa nacheza kama kiungo mshambuliaji nikitokea pembeni kushoto au kulia ni waalimu tu wenyewe wanaamua wanitumiaje kulingana na mifumo yao. Mwalimu wangu wa sasa wa Jadid ameona nafaa kwenye umaliziaji na niko vizuri kwenye movement. Aliniambia aliniona mara kadhaa na akasema anahitaji kuona uwanjani kile alichokuwa akikiona kwenye video.

Kwa hiyo katika mechi nilizocheza nimeweza kuonesha uwezo wangu na hadi sasa kwenye ile timu nacheza kama namba 10.

Nacheza nafasi yoyote ya mbele kwa sababu mimi nahitaji kufunga na pia nahitaji kutengeneza. Namba yoyote mwalimu atakayonipanga nacheza, tangu nikiwa mdogo nilikuwa nacheza namba 9 au 10.

Jezi yenye jina la mtu mwingine

Jezi zilikuwa bado hazijatengenezwa kwa sababu namba yangu haikuwepo kabisa kwa hiyo wakanipa jezi ya mtu (namba 22 ikiwa na jina ambalo si la Msuva) ambaye hakuwepo alikuwa timu ya taifa lakini kwa hiyo nikawa navaa hiyo jezi kwenye mazoezi nashukuru kwa sasa nimeletewa vifaa vyangu vipya kwa hiyo nimekabidhiwa jezi yangu namba 27.

Jezi namba 27

Niliitaka jezi namba 27 kwa sababu kwa upande wangu nilitokea kuipenda kwa sababu ya klabu yangu ya Yanga niliyokuwa naichezea kabla ya kwenda Morocco, niliitumikia vizuri kwa hiyo nilikuwa naamini itanifanya nifanye vizuri zaidi. Kiukweli haina maana yoyote ila naamini nikivaa namba 27 inanifanya nifanye kitu flani.

Lugha gongana

Ile ni nchi ya kiarabu napata tabu kuhusu suala la lugha, wenyewe wanazungumza sana Kiarabu na Kifaransa kidogo kwa upande wangu sijui Kifaransa wala kiarabu, lakini lugha ya mpira ni moja. Lugha hizo za mazungumzo nitajifunza taratibu kwa sababu nina miaka mitatu pale. Yupo phsycologist ambaye anajua kiingereza kidogo na ameniahidi kunitafutia mwalimu wa kunifundisha kiarabu na kifaransa.

Kakabidhiwa mjengo

Kule nina nyumba yangu naishi mwenyewe lakinin kuhusu mambo ya kupika, kufua na mambo mengine nimetafutiwa mtu wa kunisaidia vitu hivyo. Endapo nahitaji vitu vya ndani huwa anakwenda huyo mtu anaenisaidia au wakati mwingine huwa namwagiza huyo phsycologist lakini huwa natoka pia mwenyewe kwenda kununua vitu vidogovidogo vya ndani kwa sababu naishi karibu na shopers.

Ame-miss wali, dona

Kuna vyakula vingine nimekutana navyo kule huku nilikuwa naringa kula lakini kule hakuna jinsi inabidi nile na wao wanasisitiza kula kwa sababu wanasema vinamjenga mchezaji endapo utazingatia kula kwa wakati.

Na-miss wali kwa sababu unavyopikwa kule na huku ni tofauti lakini ugali kule hakuna, hakuna mtu anaepika ugali lakini vipo vyakula ambavyo huku pia nilikua nakula kama tambi na mikate.

Kipigo kwa Yanga Ngao ya Jamii chamvuruga

Kabla ya mchezo niliwapa hope na nilikuwa naamini timu nimeiacha vizuri na ilikuwa kwenye morali kwa upande wangu nilikuwa naamini watashinda lakini kwenye mpira kuna mambo mengi na matokeo ya mwisho Yanga walipoteza mchezo.

Kwa upande wangu niliumia na nilihuzunika kwa sababu ni timu ambayo sijatoka muda mrefu kwa hiyo nilikuwa najiona kama bado nipo Yanga kwa hiyo matokeo yaliniumiza kiukweli.

Changamoto za ugenini

Kuna na vitu vingi lakini najifunza huohumo katika nchi ya watu kwa sababu sikuwahi kuwauliza akina Samatta na Ulimwengu kuhusu walivyokuwa wanapambana na mazingira ya ugenini walivyokuwa TP Mazembe kwa hiyo ni vitu ambavyo tayari naviona na najifunza na nimeshajua natakiwa kufanya nini.

Rafiki wa nyavu za Morocco

Malengo yangu ni kusogea zaidi ya pale nilipo kwa sababu ligi yao ina ushindani mkubwa. Hadi sasa nimecheza jumla ya mechi 11,  nimefanikiwa kufunga magoli 9.

Amlilia Singano

Kwa upande wangu nilihuzunika kwa sababu tungekuwa pamoja ingekuwa kama Samatta na Ulimwengu walivyokuwa TP Mazembe kwa hiyo kungekuwa na ushirikiano ambao kila mmoja angeushangaa lakini alivyokosa nafasi nikampa moyo na yeye akanipa moyo. Kwa kuwa yeye ndio alitangulia kufika kabla yangu alinipa halihalisi ya timu wanahitaji nini.Naamini ataendelea kufanya vizuri tu na atapata timu nyingine nje ya nchi.

Kambi ya Hispania

Tulienda kuweka kambi ya maandalizi Hispania, unapozungumzia soka Hispania ni nchi ambayo Ronaldo na Messi wanacheza mpira, kwa hiyo nimejifunza vitu vingi nikiwa kule ikiwemo nidhamu ya mpira.

No comments