Breaking News

RATIBA YA SIMBA, YANGA RAUND YA PILI KOMBE LA SHIRIKISHO HII HAPA


Baada ya droo ya michuano ya Kombe laShirikisho la Azam (Azam Sports Federation Cup – ASFC), kukamilika Jumatano Desemba06, 2017 kwenye Studio za Kituo chaTelevisheni cha Azam,
kilichopo Tabata relini, Dar es Salaam,Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),limetoa ratiba rasmi ya mechi hizo za raundiya pili.

Kwa mujibu wa TFFmichuano hiyoimepangwa kucheza kwa siku tano ambazo niDesemba 20, 21, 22, 23 na 24. Mchezo kati yaSimba na Green Warriors utaochezwaDesemba 22, utakuwa ni maalumu kwa ajili yauzinduzi rasmi wa michuano hiyo msimu.Sababu Simba ndiye bingwa mtetezi.

Ratiba hiyo iliyotolewa leo Desemba 12, 2017inaonesha michezo ya Desemba 20, mwakahuu itakutanisha timu za JKT Mlale na KMC; Toto African ya Mwanza na Eleven Stars yaKagera; Ambassador na JKT Oljoro; Boma FCna NdandaMvuvumwa na JKT RuvuAbajaloitakuwa mwenyeji wa Tanzania Prisonswakati Milambo ya Tabora itachezaBuseresere ya Geita.

Desemba 21, 2017 Mshikamano itacheza naPolisi Tanzania; Rhino ya Tabora na Alliance ya MwanzaMajimaji Rangeres ya Lindiitapambana na Mbeya Kwanza ya Mbeya;Njombe Mji na Mji Mkuu ya Dodoma; Ashantina Friends Rangers za Dar es Salaam; KageraSugar na Makambako wakati Stand United yaShinyanga itacheza na AFC ya Arusha.

Desemba 22, mwaka huu kutakuwa na mechiza Green Warriors na SimbaPolisi Daritapambana na Mgambo JKT ya Tanga; Kariakoo ya Lindi na Transit Camp ya Dar ilakwa sasa imeweka maskani Shinyanga;Biashara ya Mara itacheza na MawenziMarket ya MorogoroRuvu Shooting yaMlandizi mkoani Pwani itacheza na Madini FC ya jijini Arusha huku Mufindi United na Pamba ya Mwanza ilihali Singida Uniteditacheza na Bodaboda FC.

Siku ya Desemba 23, mwaka huu Azam FC itacheza na Area C; African Lyon ya Dar es Salaam na Kiluvya United ya Pwani; Makanyagio itapambana na Mbao; Mwadui na Pepsi; Majimaji na New Generation wakatiMbeya City itacheza na Ihefu.

Desemba 24, 2017 Young Africans itacheza na Reha FC; Burkina ya Morogoro na Lipuli ya Iringa; Coastal Union ya Tanga na Dodoma FC ya Dodoma; Shupavu na Real Mojamoja wakati Villa Squad itacheza na Mtibwa Sugar ya Morogoro.

No comments