Liverpool yapendelewa kuifunga Real Madrid
Kuelekea mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, utakaopigwa Jumamosi hii kati ya Real Madrid na Liverpool, kocha Rafa Benitez amesema kikosi cha sasa cha Liverpool ni bora kuliko cha kwake cha 2005 hivyo ina nafasi kubwa ya kushinda.
''Timu yangu haikuwa bora sana ila uwezo wa mchezaji mmoja mmoja kama Steven Gerrard, Xabi Alonso na Dietmar Hamann walitufanya tuwe bora tofauti na timu ya sasa ambayo imekamilika kila idara haswa uwepo wa Mohamed Salah, Roberto Firmino na Sadio Mane,''- amesema.
Katika fainali ya Mei 25, 2005 iliyopigwa jijini Instabul Uturuki , Liverpool ilitokea nyuma na kusawazisha mabao 3 dhidi ya AC Milan kabla ya kuibuka mabingwa kupitia mikwaju ya penalti.
Washambuliaji watatu wa Liverpool msimu huu Mohamed Salah, Roberto Firmino na Sadio Mane wote kwa pamoja wamefunga zaidi ya mabao 29, huku timu nzima ikiwa imefunga mbaao 46 na kuvunja rekodi ya mabao mengi kwenye UEFA katika msimu mmoja iliyokuwa ikishikiliwa na Barcelona (45).
No comments