Hans Van Der Pluijm kutua Azam FC kumrithi Mromania
Taarifa za chini ya kapeti zinaeleza kuwa uongozi wa klabu ya Azam FC unaweza ukaachana na Kocha wake Mromania, Aristica Cioaba, huku Mholanzi, Hans van der Pluijm akitajwa kurithi mikoba yake.
Inaelezwa Azam wamefikia hatua hiyo kutokana na timu yao kushindwa kufanya vizuri ndani ya misimu miwili mfululizo na ikishindwa kutwaa taji lolote lile.
Kocha Pluijm ambaye anaiona Singida United ya mjini Singida hivi sasa anatajwa kama mbadala wake mkubwa na inavyoonekana anaweza akasainiwa na matajiri hao wa jiji la Dar es Salaam siku kadhaa zijazo.
Kikosi cha Azam kimeshindwa kufanya vizuri msimu huu ambapo tayari kimeshaondolewa katika mashindano ya Kombe la Shirikisho kwa changamoto ya mikwaju ya penati dhidi ya Mtibwa Sugar.
Mbali na kuondolewa huko, mpaka sasa timu hiyo ipo katika nafasi ya tatu ya msimamo wa ligi ikiwa imejikusanyia alama 45 huku ikicheza michezo 23.
No comments