Natukanwa Sana, Nashambuliwa Kisa Mke wangu – Roma Mkatoliki
Msanii wa muziki wa Hip Hop, Roma Mkatoliki amefunguka kwa kudai kuwa baada ya mama watoto wake kumpambania katika matatizo ya kutekwa miezi miwili iliyopita, mashabiki hawataki kuona rapa huyo akifanyia tendo lolote baya mwanamke huyo.
Rapa huyo amedai akionekana anapiga picha na mwanamke yeyote tofauti na mke wake huyo anaoga matusi kupitia mitandao ya kijamii kitu ambacho kinamfanya aishi kwa taadhari.
“Natukanwa, nashambuliwa sana tena nikionekana nipo na mwanamke tunatembea maeneo fulani natukanwa sana, wanasema wewe mwanamke wako alivyokupambania halafu unafanya ushenzi,” Roma aliimbia Bongo5. “Kwa hiyo inaonekana ni mwanamke fulani aliyebarikiwa na hatakiwi kukosewa kabisa,”
Katika hatua nyingine rapa huyo amedai bado kidole chake kimoja hakijakaa sawa mpaka sasa baada ya kuteguka miezi miwili iliyopita baada ya kutekwa na watu wasiojulikana.
No comments