YANGA WAIENDEA SIMBA PEMBA
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu bara Yanga wameamua kufunga safari na kwenda Kisiwani Pemba Zanzibar kwa ajili ya maandalizi ya wiki moja kujipanga kuikabili klabu ya Simba katika mchezo wa Ngao ya jamii utakayochezwa tarehe 23 Agosti Dar es Saalam.
Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa amesema kuwa kikosi chake kitaondoka jijini Dar es Salaam baada ya mechi yao dhidi ya Ruvu Shooting itakayochezwa Jumamosi Uwanja wa Taifa na kwenda Zanzibar kwa mechi ya pili itakayochezwa Jumapili na baada ya mechi hiyo kikosi cha Yanga kitapiga kambi ya wiki nzima kisiwani humu kujipanda kwa ajili ya mchezo wa ngao ya jamii.
"Mara baada ya mchezo dhidi ya Mlandege FC katika uwanja wa Amani siku ya Jumapili, kikosi chetu kitaelekea Pemba kuweka kambi kujiandaa na mchezo wa Ngao ya Jamii itakayochezwa tarehe 23 Agosti mwaka huu" alisema Mkwasa
Klabu ya Simba na Yanga zitakutana katika mchezo wa Ngao ya jamii kama ishara ya ufunguzi wa mashindano ya Ligi Kuu Tanzania Bara 2017/2018 mchezo ambao unatarajiwa kuwa na mvuto wa aina yake kutokana na klabu hizi mbili zote kujipanda kisawasawa katika msimu huu
No comments