Shetta Aonyesha Urijali Wake
Msanii wa muziki wa bongo fleva Nurdin Bilal maarufu kwa jina la Shetta, ameonyesha urijali wake kwa kubahatika kupata mtoto wa pili aliyezaliwa leo.
Kwenye ukurasa wake wa instagram Shetta amepost picha akiwa amebeba kichanga huku akiandika maneno ya kumkaribisha mtoto huyo duniani.
"Karibu duniani mwanangu....!! Asante Mungu kwa huyu mwingine, sasa Kayla uache kuringa", ameandika Shetta.
Kufuatia kuzaliwa kwa mtoto huyo Shetta atakuwa na watoto wawili, ambapo wa kwanza anaitwa Kayla.
No comments