Mtoto Anayeishi kwa Kunywa Mafuta Apata Ahueni
Dkt. Sufiana Rwezaura akizungumza na wanahabari
DAR ES SALAAM: Mtoto ambaye amekuwa akiishi kwa kunywa mafuta ya kula na kula sukari, Shukrani Kipango, alilazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili amefanyiwa vipimo na kukutwa na tatizo la sikoseli pamoja na upungufu wa madini ya chuma ambayo yamesababishwa na kutokula vyakula vya vitamini ili kumsaidia kutengeneza damu .
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo daktari bingwa wa magonjwa ya damu na Mkuu wa Kitengo cha Magonjwa ya Damu katika hospitali hiyo, Sufiana Rwezaura amesema kuwa ugonjwa huo ameurithi kutoka kwa wazazi wote wawili.
Dkt. Rwezaura amebainisha kuwa tatizo la sikoseli husababisha chembechembe nyekundu za damu kuwa na upungufu wa oksijeni kwenye damu, anapopata maambukizi yoyote zinabadilika na kuwa katika umbo la duara (selimundu) na zinapokuwa katika umbo hilo mwili unaziharibu kwa haraka na kupelekea upungufu wa damu mara kwa mara.
Amesema kuwa chembechembe hizo zikiharibiwa kwa wingi zinatengeneza nyongo ambayo husambaa kwenye mwilini na kuleta rangi ya njano au nyeupe.
Aidha amesema kuwa tatizo la kuvimba kichwa na maumivu makali linatokana na chembechembe nyekundu zinapobadilika na kuwa katika umbo la selimundu haziwezi kupita katika mishipa midogo ya damu na kusababisha damu kushindwa kutembea kwenda upande wa pili na kuleta uvimbe mwilini.
Mama wa mtoto Shukuru, Mwanabibi Mtei
Naye mama wa mtoto Shukuru, Mwanabibi Mtei ameeleza namna ambavyo mwanaye ambavyo amekuwa akiteseka kwa maumivu na kubadilika rangi ya ngozi.
Mtoto Shukuru
Aidha mama huyo amewashukuru madaktari wa Muhimbili, serikali na wizara ya afya kwa kumsaidia mwanaye ambaye sasa anaendelea vizuri bila kula mafuta wala sukari tena.
No comments