Breaking News

KAMA HUJUI HIZI NDIZO FAIDA ZA KUTEMBEA KWA MIGUU


Mtindo wa maisha unawafanya wengi kutumia magari au usafiri wa aina nyingine hata katika eneo la umbali mfupi.

Kama wazee wetu walivyoishi kwa kutembea hata sisi tunajionea jinsi walivyo wakakamavu na walivyoishi muda mrefu. Miongoni mwa mazoezi mepesi na yasiyo na masharti makubwa ni yale ya kutembea. Kutembea ni njia rahisi za kufanya mazoezi.

Huhitaji vipimo vya afya kuweza kufanya zoezi hili na badala yake unahitaji mavazi yasiyokwaza, pamoja na mahali pa kutembelea.

Wakati wataalamu wa afya wanapendekeza kupata ushauri wa daktari kabla ya kuanza kufanya mazoezi magumu, lakini mazoezi mepesi yanashauriwa kwa mtu yeyote na mahali popote.

Wataalam wa masuala ya afya, wanasema kutembea ni njia salama na nzuri inayosaidia kuujenga na kuuimarisha moyo uwe na afya nzuri na usio katika hatari ya kushambuliwa na maradhi. Kiongozi wa mazoezi katika Gym ya ‘Fitness Mobb’ Sinza , Zakaria Malya anasema mazoezi au tabia ya kufanya mazoezi inayo faida kubwa zaidi kuliko matumizi ya dawa.

Kutembea ni moja ya mazoezi yanayohimizwa kufanya na yanayoweza kusaidia kujenga afya ya mwili.

Wataalamu wa masuala ya afya na magonjwa ya moyo wanasema kutembea ni miongoni mwa kinga ya mwili kushambuliwa na magonjwa mbalimbali ukiwemo wa moyo na kiharusi.

Kutembea vile vile ni tiba kwa mtu mwenye kusumbuliwa na matatizo ya ubongo na kwamba, badala ya kujenga tabia ya kutumia dawa za kupunguza msongo wa mawazo, ni vyema mtu mwenye tatizo hilo akajenga tabia ya kutembea kwa dakika 20-30 kila siku.

Kutembea kunazuia ugonjwa wa kisukari kutokana na mazoezi hayo kuboresha uwezo wa mwili wa kutumia tezi ya insulini.

Kutembea vilevile kunaiweka mifupa kuwa imara na kuikinga na mashambulizi ya kuzuia ugonjwa wa mifupa. Kutembea kunasaidia kupunguza uzito unaoongezeka bila mpangilio.


No comments