HISTORIA FUPI YA STEVEN KANUMBA
Steven Charles Kanumbaa alizaliwa Januari 8, mwaka 1984 mkoani Shinyanga.
Alipata elimu ya msingi katika shule ya Bugoyi, na kisha kujiunga na sekondari ya Mwadui mkoani Shinyanga na baadaye alihamia Dar Christian Seminary.
Aliendelea na masomo ya kitado cha tano na sita katika shule sekondari ya Jitegemee, Dar es Salaam.
KUANZA KWA SHUGHULI ZA SANAA:
Akiwa katika shule ya Jitegemee Kanumba alianza shughuli za sanaa ndani ya Kundi la Kaole Sanaa Group la Magomeni, Dar es Salaam.
Baada ya kupata uzoefu wa kutosha na kundi la Kaole, Kanumba aliamua kuanzisha kampuni yake ya filamu ambayo alikuwa anaiongoza mpaka umauti unamkuta. Umahiri wa uingizaji wake ulimfanya afahamike kila pande za bara la Afrika kama vile Nigeria, Ghana,DRC, Kenya, Uganda na kwengineko nje na ndani ya bara la Afrika.
WASANII WA KIMATAIFA ALIOSHIRIKIANA NAO:
Ameshirikiana na wasanii wakubwa duniani kama Ramsey Nouah wa Nigeria. Mbali na hao marehemu pia alibahatika kucheza filamu na mastaa wengine kadhaa kutoka nchini Nigeria.
Miongoni mwa filamu alizocheza Kanumba na kumpa umaarufu ni Dar To Lagos, She is My Sister, Ancle JJ, Oprah, Tufani, Johari, Gharika, Baragumu, Sikitiko Langu, Dangerous Desire, Cross My Sin, Village Pastor, Family Tears na nyingine nyingi.
SIASA:
Kanumba alikuwa anajihusisha na mambo ya siasa chini kwa chini na hivi karibuni, alikaririwa akisema atagombea Ubunge katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015.
Kama haukuwahi fahamu kanumba alikuwa ana kipaji cha musiki pia
Alikuwa Mwanaspoti
Moja ya matukio katika timu ya Bongo Movie
Moja ya matukio katika kazi zake za usanii wa filamu
Mwigizaji maarufu wa filamu hapa nchini Marehemu Steven Kanumba (kulia) akiwa na mwigizaji kutoka nchini Nigeria Ramsey Noah katika hotel ya Peacock wakati walipozungumza na waandishi wa habari kuhusu ujio na ushiriki wa Ramsey Noah katika filamu mpya ya Devil Kingdom ilyoigizwa na Steven Kanumba kwa kushiriana na Muigizaji huyo maarufu kutoka NigeriaKanumba akiwa ndani ya duka la B&H New york
Marehemu Kanumba Akicheza Musiki
Marehem Steven Kanumba alivyomtembelea Mzee Kipara
Marehemu Kanumba Akimkabidhi fedha Marehemu Mzee Kipara
Akimfariji marehem mzee kiparaMarehemu Steven Kanumba akiwa na Rais Jakaya Kikwete
No comments