Breaking News

Mahakama Imeruhusu Polisi Kumuhoji Manji na Wenzake Ili Kukamilisha Upelelezi


 Mahakàma ya Hakimu Mkazi Kisutu imeruhusu Mfanyabiashara Yusuf Manji na wenzake wahojiwe na Polisi ili kukamilisha upelelezi wa kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili.

Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi ambapo amesema ameruhusu washtakiwa wahojiwe baada ya kuandikiwa barua na Mkuu wa Upelelezi (ZCO).

”Hivyo nikisema Mahakama izuie wasihojiwe itakuwa tunapingana nao, wakati kila siku tunapigiana kelele kuhusu upelelezi kukamilika. Hivyo, sifikirii kesi hii kila siku iwe inatajwa tu.”

Hakimu Shahidi alimkabidhi Manji na washtakiwa wenzake kwa Koplo Dotto ambapo amemtaka hadi kesho kwenye muda wa kazi wawe wamerudishwa Mahakamani.

Mbali ya Manji washtakiwa wengine ni Deogratius Kisinda, Abdallah Sangey na Thobias Fwer

No comments