Breaking News

MABADILIKO YAMTIBUA LWANDANINA


Kocha Mkuu wa Yanga, George Lwandamina amechoshwa na kitendo Shirikisho la mpira wa Miguu Tanzania TFF kubadili mara kwa mara ratiba ya Ligi Kuu Tanzania bara na kusema kitendo hicho kinaathiri utaratibu wa klabu hiyo.

Lwandamina amesema hayo kupitia katika ukurasa wa facebook wa Yanga na kusema kuwa timu yake leo ilipaswa kusafiri na kuelekea mjini Njombe ambapo ilitakiwa icheze na klabu ya Njombe Mji Septemba 6 baada ya ratiba ya awali kubadilishwa ambapo walitakiwa kukutana Septemba 3, 2017.

"Inasikitisha kuona ratiba ya ligi ikibadilika mara kwa mara, jambo hili lina athari kubwa, tulipanga kusafiri leo kwa ajili ya mchezo wa tarehe 6,lakini sasa tunalazimika kuongeza siku zaidi, hii ina maana kuwa 'program' zote zilizowekwa awali zinavurugika"  alisema George Lwandamina.

Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania (TFF) imefanya mabadiliko ya ratiba ya Ligi Kuu Tanzania bara 2017/2018 kwa mara ya tatu ambapo sasa michezo yote ambayo ilipaswa kucheza Jumatano ya wiki hii itachezwa siku ya Jumamosi Septemba 9, 2017 na baada ya hapo ndipo itatoa ratiba nyingine ya Ligi Kuu Tanzania Bara 2017/2018

No comments