Breaking News

WAPO WABUNGE HAWANA VYETI VYA KUZALIWA

Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi amesema wapo wabunge ambao bado hawajasajiliwa na Wakala wa Vizazi na Vifo (Rita).

Profesa Kabudi ameyasema hayo leo (Jumamosi) katika semina ya wahariri wa vyombo vya habari nchini, inayofanyika Morogoro.

“Nitahakikisha ninasimamia hilo na wabunge wote watasajiliwa,” amesema.

Rita ndiyo wanaotoa vyeti vya kuzaliwa na baada ya kifo, hutoa cheti cha kifo.

Profesa Kabudi mbaye ni mgeni rasmi katika semina hiyo, pia amesema watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano kutoka katika mikoa minne nchini wamesajiliwa kwa asilimia 100.

Ameitaja mikoa hiyo kuwa ni Njombe, Iringa, Geita na Shinyanga.

 Kadhalika, Mwenyekiti wa Bodi ya Rita, Profesa Hamis Dihenga amesema ni asilimia 13 tu ya watu nchini ambao wamesajiliwa na wakala huo.

 Idadi hiyo inamaanisha kuwa, kuna asilimia 87 ya watu ambao bado hawajasajiliwa na wakala huo.

No comments