Breaking News

KUPITILIZA SIKU ZA KUJIFUNGUA KWA MJAMZITO(OVERDUE PREGNANCY)

Mama mjamzito anapopitiliza siku za kujifungua kwenye wiki ya 40 ,anakosa amani na kujiuliza maswali mengi. Mimba ikifika wiki 41-42 hapo inakuwa imepitiliza muda  (overdue).

Kuna sababu tofauti zinazo sababisha mama kupitiliza siku zake za kujifungua.
Baadhi ya sababu za kupitiliza kujifungua ‘overdue’:

1. Iwapo mama atahesabu siku zake vibaya basi hapo ataona amepitiza siku za kujifungua

2. Kama ulishazaa kwa mara ya kwanza na ukapitiliza

   basi uzao wako unaofuata  tatizo linaweza kujirudia.

3. Kupitiliza kujifungua pia hurithiwa kutoka kwa  familia.

4. Watoto wa kiume mara nyingi  huchelewa kutoka tofauti na wa kike.

5. Matatizo ya kondo la uzazi kushindwa fanya kazi ipasavyo.

MADHARA YANAYO JITOKEZA MAMA ANAPOPITILIZA SIKU ZA KUJIFUNGUA

Mimba inapokuwa zaidi ya wiki 41, afya ya mtoto inakuwa hatarini kama ifuatavyo:

1. Mtoto anaweza kupata choo (kujisaidia) na kula kinyesi akiwa tumboni.

2. Kupungua kwa kiwango cha maji yanayomzunguka mtoto (ambiotic fluid).

3. Mapigo ya moyo ya mtoto kupungua.

4.Mama anaweza  kuzaa kwa c-section sababu mtoto kesha kuwa mkubwa.

MAMA ANATAKIWA KUFANYA NINI?

Mama anapopitiliza kujifungua anahitaji kuwa karibu na daktari mara kwa mara. Iwapo utapata dalili yoyote usiyoielewa, wahi hospitali.


No comments