Breaking News

Lampard: Lukaku anastahili kumbadili Costa, Chelsea

Mchezaji wa zamani wa Chelsea, Frank Lampard amesema anaamini Romelu Lukaku ndiye chaguo sahihi kwa klabu hiyo ili kumbadili Diego Costa. 

Hata hivyo, anaamini kwamba kuondoka kwa mchezaji huyo raia wa Hispania kutawashtua wengi. 

Hivi karibuni Costa alimlalamikia kocha wake, Antonio Conte kuwa hamhitaji kwenye klabu hiyo mabingwa wa Ligi Kuu England 2016/17. 

Costa amefanikiwa kufunga mabao 22 kwenye msimu ulioisha. 

Lukaku mwenye miaka 24 amekuwa akihusishwa kuhamia dimba la Stamford Bridge akiwa ameitumikia Everton kwa misimu minne yenye mafanikio.

No comments