Taarifa kutoka IKULU Dar es salaam asubuhi hii
May 24, 2017
Kutoka Ikulu Dar es salaam asubuhi hii Vyombo vya habari vimepokea taarifa hii kutoka kwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais IKULU Gerson Msigwa.
Taarifa hiyo iliyosambazwa saa kumi na mbili kasoro ni kuhusu uteuzi uliofanywa leo May 24 2017 na Rais Magufuli ambapo Tixon Tuliangine Nzunda ameteuliwa kuwa Naibu katibu mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) anaeshughulikia Elimu.
Kabla ya uteuzi huo Tixon alikua Katibu tawala wa mkoa wa Rukwa ambapo anakuja kuchukua nafasi ya Benard Makali ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa mkoa wa Rukwa na uteuzi huu unaanza mara moja.
No comments