JULIUS MTATIRO "TAIFA LILIMPOTEZA NYERERE, LIMEMZIKA KINGUNE
Taifa lilimpoteza Julius Nyerere, taifalimempoteza Kingunge! Kamaunafuatilia historia ya taifa letu lazimautakuwa unajua kuwa ni mara chachesana taifa lolote linakuwa na wanasiasawa haiba hiyo.
Taifa limekuwa na mamia na maelfu yawanasiasa, lakini Nyerere na Kingungeni EXCEPTIONAL! Na ukitafuta haowanasiasa mahsusi na wa kipekee kwasasa, ni kwa tochi!
Kingunge hakuwa mwanasiasa tu,alikuwa ni STRATEGIST wa hali ya juu.Nakumbuka siku niliyokutana naye anakwa ana kwa mara ya kwanza nyumbanikwake, ilikuwa miaka 10 iliyopita.
Mimi na wenzangu tulikuwa kwakekumshawishi azungumze na Rais iliserikali ione haja ya kuongeza pesa zakujikimu za wanafunzi. Kikao kilekilikwenda jioni nzima na akakihamishakesho yake asubuhi.
Mara ya pili kwenda kwake ilikuwa nikuzungumza naye juu ya namna serikaliilivyokosea kutatua mgogoro baina yakena wanafunzi wa UDSM. Mwita Waitara,Mbunge wa Ukonga anaikumbuka ziarahii vizuri sana.
Mzee Kingunge anakusikiliza dakika 15 au ukipenda dakika 30, unazungumzawewe tu, ukimaliza, anaanza kupitiahoja zako zote na anazigeuzageuzaanavyotaka.
Anakuonesha makosa ya serikali,anakueleza makosa ya wanafunzi,anakidadavulia uchuro wa uongozi wachuo kisha anakwambia atakwendakuzungumza jambo gani na Rais!
Leo hii hakuna BRAINS kama za Nyerere na Kingunge. Leo kuna hizi BRAINS zetu, za kawaida kabisa, za COPYING and PASTING, za kufoka na kutukana na kupiga risasi na kutisha na kuzuia na kutweza na kuumiza, kunyima dhamana na kufunga, kutafuta ukuu na kutafuta sifa.
Nitakuwa na fursa ya kueleza mengi kwa kina kuhusu ziara mbili ambazo nilishiriki na kuzungumza na mzee huyu muhimu kwa kirefu, nitafanya hivyo kwa njia maalum sana.
Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.
Mungu atusaidie tujenge hata robo tu ya uwezo aliokuwa nao Mzee wa taifa.
No comments