Breaking News

KUTANA NA MCHEZAJI AMBAE NDANI YA MISIMU MIWILI MCHEZAJI AMEPANDISHA TIMU MBIL

I

Songa Betheli ni mshambuliajiliyeweka rekodi ya kupandisha ligi kuutimu mbili kwa misimu miwili tofauti,msimu uliopita aliisaidia Singida Unitedkupanda daraja kchoamekifanya tena akiwa na BiasharaUnited ya Musoma mkoani Mara.

Betheli ni miongoni mwa wachezajiwalioisaidia singida kupada ligi kuu kwakufungia magoli mengi timu hiyo lakinibaada ya minziro kuondoka SingidaUnited betheli aliondoka pia.

“Kwa sasa ni mchezaji wa BiasharaUnited ambayo tumefanikiwakuipandisha ligi kuu baada ya kazingumu lakini napenda kumshukuruMungu kwa hiloNikilinganisha furahaniliyokuwanayo nikiwa Singida United nitofauti na hapa Biashara kwa sababunikiwa hapa nimeweza kuwa namahusiano mazuri na wachezajiwenzangubenchi la ufundi pamoja nauongozi mzima hiyo ndiyo tofauti nanilivyokuwa Singida United.”

“Nina uwezo ndio maana nakuwakwenye timu na ninakuwa na mchangowa kufanikisha timu kupanda daraja,malengo yangu kwa sasa ni kucheza ligi kuu kwa kwa mafanikio kwa sababu umri haunisubiri.”

“Niliamua kutoka Singida United nikaenda Stand United lakini nikajiunga na Biashara katika dirisha dogo ili nije nijifue nifanye vizuri lakini pia nipate ‘title’, malengo yangu niliyojiwekea katika michezo mitano nikiwa Biashara nimeyatimiza, nimefunga magoli manne katika mechi tano nilizocheza, mchezo wa mwisho dhidi ya Transit Camp nimehusika katika magoli yote matatu tuliyofunga. Nimesababisha penati tukafunga goli la kwanza, nikafunga mwenyewe goli la pili nikatoa assist ya goli la tatu.”

“Mipango yangu ilikuwa kuja biashara kwa ajili ya kujifua lakini kwa sasa nitaipa kipaumbele Bishara kwa maana timu nitakayoichezea ligi kuu kama watakuwa tayari kukaa na mimi na kunipa mkataba.”

Songa anaungana na aliyekuwa kocha wake Singida United Fred Felix Minziro ambaye pia ameweka rekodi ya kupandisha ligi guu timu mbili tofauti katika misimu miwili mfululizo.

Mkoa wa Mara utashudia michezo ya ligi kuu Tanzania bara baada ya Biashara United kupanda ligi kuu kutokana na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya transit camp kwenye mchezo wa mwisho wa Kundi C uliochezwa uwanja wa Karume mjini Musoma.

No comments