CHELSEA YALAZWA 4-1 NA WATFORD
Watford ilifunga mabao matatu ya dakika za lala salama kushinda mechi ya kwanza ya mkufunzi Javi Gracia dhidi ya Chelsea.
Watford ilifunga mabao matatu ya dakika za lala salama kushinda mechi ya kwanza ya mkufunzi Javi Gracia dhidi ya Chelsea ,ushindi unaompatia shinikizo kali mwenzake wa Chelsea Antonio Conte.
Chelsea ilicheza takriban saa moja ikiwa na wachezaji 10 baada ya Tiemoue Bakayoko kupewa kadi nyekundu baada ya kucheza visivyo hatua ilioipatia Watford fursa ya kufunga mabao manne.
The Hornets ambao walikuwa wamepata ushindi mmoja kati ya mechi 12 walizocheza waliongoza kwa utata baada ya Gerard Deulofue kujiangusha kwa urahisi kufuatia kabiliano la kipa Thibaut Courtois huku Troy Deeney akifunga mkwaju wa penalti.
Chelsea iliomuingiza Olivier Giroud kwa mechi yake ya kwanza katika kipindi cha pili ilisawazisha wakati nyota wao Eden Hazard alipofunga bao zuri akiwa miguu 25 kutoka kwa lango.
Lakini dakika mbili baadaye ,Daryl Janmaat alifunga bao zuri wakati alipochenga kutoka wingi ya kulia na kucheza moja mbili na Robert Pereyra akawachenga mabeki wengine kabla ya kufunga na mguu wake wa kushoto.
Deulofeu aliongeza bao lake la pili wakati alipotamba na mpira na kushambulia kabla ya mpira kumpiga beki Gary Cahill na kuingia.
Watford sasa wako pointi sita juu ya eneo la kushushwa daraja.Gracia ambaye alichukua mahala pake marco Silva mwezi uliopita aliambia bbc Sport: Ulikuwa ushindi mkubwa na mechi nzuri, Nawapongeza wachezaji wangu.Tulicheza mechi nzuri , tukawasukuma sana.
''Mechi ilibailika baada ya kadi nyekundu kutolewa lakini nadhani tulicheza vyema. Chel;sea ni klabu kubwa sana , na timu kubwa''.
No comments