FAHAMU JINSI YA KUPATA MTOTO WA JINSIA UNAYOTAKA
Mchakato mzima wa uzazi huwa ni bahati tu.Bahati kubeba mimba,bahati kupata mapacha na bahati kupata jinsia ya mtoto unayemtaka.Uwezekano wa kupata mtoto wa kike au wa kiume ni nusu kwa nusu.Lakini kuna njia yenye mshiko inayoweza kukusaidia kupata mtoto wa jinsia unayotaka.
Zingatia hili
Kwenye kila shahawa mwanaume anazotoa kuna mamilioni ya mbegu zinazobeba watoto wa kiume na mamilioni ya mbegu zinazobeba watoto wa kike.Kutoka kwenye mamilioni hayo ya mbegu,ni mbegu moja tu ya mwanaume inayowahi mapema kulifikia yai la mwanamke na kutungisha mimba.Kama mbegu iliyobeba mtoto wa kiume ndiyo itawahi kufika kwenye yai basi mtoto wa kiume atapatikana,kama mbegu iliyobeba mtoto wa kike ndiyo itawahi kufika kwenye yai basi mtoto wa kike atapatikana.
Kanuni kuu ya njia hii
Kwenye kila lundo la shahawa,mbegu zinazobeba watoto wa kiume huwa zina kasi(mbio) sana lakini hazina maisha marefu(huishi mpaka siku 2 ndani ya mwili wa mwanamke).Mbegu(shahawa) zinazobeba watoto wa kike huwa hazina kasi(mbio) kubwa lakini zikiwa mwilini mwa mwanamke zinaishi mpaka kufikia siku nne,zina maisha marefu kuliko zile zinazobeba watoto wa kiume.
Jinsi ya kupata mtoto wa kiume
Mtoto wa kiume atapatikana iwapo mwanamke atafanya mapenzi akiwa kwenye siku zake hatarishi zaidi(siku za kubeba mimba).Katika siku hatarishi,yai la mwanamke tayari linakuwa limefika kwenye mji wa mimba linasubiri mbegu za kiume(shahawa).Kumbuka kuwa,kwenye shahawa mbegu zilizobeba watoto wa kiume ndizo zenye kasi zaidi,hivyo zitawahi kufika kwenye mji wa mimba,zitakuta yai na kulitungisha mimba,hivyo mtoto wa kiume atapatikana.
Jinsi ya kupata mtoto wa kike
Mtoto wa kike atapatikana iwapo mwanamke atafanya mapenzi siku chache(siku 2 mpaka 4) kabla ya kuingia kwenye siku zake hatarishi(siku zisizo za kubeba mimba).Katika siku hizi ambazo sio hatarishi yai la mwanamke linakuwa halijafika kwenye mji wa mimba.Kwa kuwa mbegu za mwanaume(shahawa) zinazobeba mtoto wa kiume zina kasi zaidi zitawahi kufika kwenye mji wa mimba.Zikifika kwenye mji wa mimba zinakuta hakuna yai....Kwa upande mwingine mbegu zilizobeba watoto wa kike,kwa kuwa zina kasi ndogo,zitachelewa kufika kwenye mji wa mimba.Zikifika kwenye mji wa mimba zitakuta tayari mbegu zinazobeba watoto wa kiume zimeshafika,na zenyewe pia(mbegu zilizobeba watoto wa kike) zitakakaa hapo zikisubiri yai.Kwa kuwa mbegu zilizobeba watoto wa kiume zina maisha mafupi hufa baada ya siku chache(siku mbili) na kuziacha mbegu zilizobeba watoto wa kike pekee.Kwa kuwa tendo la ndoa litakuwa limefanyika siku chache(siku 2 mpaka 4) kabla ya yai kufika mji wa mimba(siku zisizo za kubeba mimba),siku chache baadae yai litakaporuhusiwa kufika kwenye mji wa mimba litakuta mbegu zilizobeba watoto wa kiume tayari zimekufa,mbegu zilizobeba watoto wa kike zipo peke yake hivyo zitatungisha mimba na mtoto wa kike atapatikana.
Kwa kuwa uzazi ni mchezo wa bahati hakuna uhakika wa asilimia mia moja kuwa njia hii itakupatia mtoto wa jinsia unayotaka.Lakini huna cha kupoteza ukijaribu njia hii.

No comments