Breaking News

MWENYEKITI UVCCM ARUSHA AKAMATWA NA POLISI

Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Arusha ambaye pia ni Diwani wa kata ya Sambasha Halmashauri ya wilaya Arusha kupitia chama cha Mapinduzi Mh Lengai Ole Sabaya anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Arusha tokea saa moja asubuhi ya leo tarehe 10/8/2017 katika kituo kikuu cha polisi Mjini Arusha.

Taarifa zinadai Diwani huyo amekamatwa na Jeshi la Polisi kwa agizo la Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh. Mrisho Gambo kutokana na tofauti zao za kisiasa mkoani hapo.

Tofauti hizo zinatokana Mwenyenyekiti huyo wa UVCCM Mkoa kumuunga mkono Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mh Alexander Mnyeti kutokana Mkuu huyo wa wilaya kutofautiana na Mkuu wa mkoa.

Hivi karibuni inadaiwa kuwa Mkuu wa mkoa alimfukuza DC katika kikao cha kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Arumeru kilichofanyika katika ukumbi wa mkutano wa Halmashauri ya Arusha baada ya Mkuu wa wilaya kuchelewa kuwasili kikaoni na kutanguliwa na Mkuu wa mkoa ambapo Mkuu wa mkoa alimwagiza Mkuu wa Wilaya aandike barua kwake kwanini asifukuzwe kazi kwa kitendo cha kuchelewa.

Inadaiwa Lengai Ole Sabaya alimpinga Mkuu wa mkoa adharani kitendo kilichomkwaza Rc Gambo na sasa ameamua kufufua kesi iliyokwisha kufutwa na mahakama kwa Jamhuri kukosa ushahidi.

Bado polisi wanamshikilia diwani huyo kwa sasa wanadai watampeleka mahakamani upelelezi utakapokamilika.

No comments