BILL GATES AMTEMBELEA MAGUFULI
Bill Gates amemtembelea Rais Magufuli ikulu jijini Dar na kufanya mazungumzo naye ambapo pamoja na mambo mengine taasisi ya Bill Gates imetenga bilioni 777 kwa ajili ya kusaidia miradi mbalimbali ikiwemo afya, kilimo na huduma za kielektroniki ili kurahisisha upatikanaji wa taarifa nchini.
Aidha Bill Gates ambaye pia ni taijiri nambari moja duniani ameeleza kufurahishwa na hatua zinazochukuliwa na Rais Magufuli katika kupambana na rushwa, ufisadi na uhujumu uchumi katika kuwaletea wananchi maendeleo.
Ujio wa Bill Gates ni muendelezo wa kuwaaibisha wale waliokuwa wameandika barua kwa wahisani akiwemo Bill Gates ili Tanzania inyimwe misaada hususani misaada katika sekta ya afya.
No comments