Serikali Yakichukua kiwanda cha Ngozi Africa Tanneries, Mwanza
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekichukua kiwanda cha kusindika ngozi cha Mwanza Tanneries kilichopo eneo la viwanda Ilemela mkaoni Mwanza kutokana na kushindwa kuendelezwa na wamiliki wake toka mwaka 1998.
Mkuu wa Mkoa Mwanza John Mongella ameamuru makampuni ya Skysraper na Caspian kurudisha funguo za kiwanda cha Ngozi Africa Tanneries Limited Mwanza kwa Serikali na kuwa mali ya Serikali rasmi.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella ametangaza uamuzi huo kutokana na wawekezaji wa kiwanda hicho kushindwa kukuendeleza lakini pia kuwepo kwa udanganyifu wa umiliki wa kiwanda hicho uliodaiwa kufanya na kampuni ya Quality Group.
Mongella ametangaza maamuzi hayo mbele ya Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa huo, wakiwemo pia wawakilishi wa kampuni ya Caspian na Quality Group zilizoshindwa kutekeleza masharti ya mkataba wa kukiendeleza kiwanda hicho toka mwaka 1998.
No comments