Breaking News

Wabunge wawapongeza watoto wa Kikwete, Nkamia



Wanafunzi watatu walioshinda tuzo ya Genius Olympiad huko Marekani wametambulishwa bungeni jana kwa kuliletea Taifa heshima. 

Wanafunzi hao kutoka Sekondari ya Wavulana ya Feza jijini Dar es Salaam waliambatana na walimu wao wawili. Walikuja bungeni kwa mwaliko wa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako. 

Spika wa Bunge, Job Ndugai aliwatambulisha wageni watano wa Profesa Ndalichako wakiwamo walimu wawili na wanafunzi watatu walioshinda medali za dhahabu katika mashindano ya kimataifa ya mazingira na sayansi yaliyofanyika. 

“Tunawapongeza kwa kushinda tuzo hizo. Mmepeperusha bendera ya Tanzania vizuri sana,” alisema Ndugai. 

Aliwataja wanafunzi hao kuwa ni Abdallah Rubeya, Abdularazak Juma Nkamia ambaye ni mtoto wa Mbunge wa Chemba, Juma Nkamia na Khalifan Jakaya Kikwete, mtoto wa Rais mstaafu, Jakaya Kikwete. 

Hakusita kutania na kuwapongeza wazazi wa watoto hao kwa kusema: “Kutoka Chemba mpaka Marekani na kufanya mambo kule, kumbe inawezekana haya mambo. Lakini, hongera sana kwa Mama Salma Kikwete kwa sababu yupo Khalfan Jakaya Kikwete.” 

Kukaribishwa kwao bungeni ni sehemu ya juhudi za Serikali kuwatambua wanafunzi wanaofanya vizuri kwenye masomo yao ili kuwaongezea morali na kuwahamasisha wengine waliopo kwenye ngazi tofauti shuleni na vyuoni pia. 

Hivi karibuni, watoto hao walipokelewa kishujaa na ndugu, jamaa na marafiki waliojitokeza Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam kabla hawajaletwa bungeni jana. 

Walioongozana na wanafunzi hao ni mkurugenzi pamoja na mkuu wa shule hiyo

No comments