MBINU ZA KUONGEZA VIWANGO VYA UFAULU WA MITIHANI YA TAIFA KWA WANAFUNZI WA ELIMU YA MSINGI NA SEKONDARI NCHINI.
Na MP Esrom Fubusa
Naziunga mkono jitihada zinazofanywa na mkuu Wa mkoa Wa Dar es salaam {RC Paul Makonda} za kuhakikisha viwango vya elimu vinaongezeka katika ufaulu Wa wanafunzi Wa elimu ya msingi na sekondari katika matokeo ya Mitihani ya taifa.
Sambamba na hilo, nadhani hajatafiti ni wapi mchawi Wa elimu ya Tanzania alipojificha, kitendo cha kuwataka maafisa elimu Wa manispaa na halimashauri kutoa maelezo kwa njia ya maandishi ama kuacha kazi au kutoa maelezo juu ya mbinu watakazozitumia ili kuhakikisha elimu ya Tanzania inaimarika kwa kiwango cha juu,
Maafisa elimu wao ni wasimamizi tu Wa maswala ya kielimu katika halimashauri na manispaa zao nchini., ni kweli maafisa elimu wamejitahidi sana katika kuhakikisha wanapata vitendea kazi katika shule zilizopo katika halimashauri na manispaa zao lakini kulingana na fungu la fedha linalotolewa na serikali inawawia vigumu kufanikisha mipango yao.
Shuleni kumekua na uhaba wa vitabu vya kiada na ziada ambavyo vitawafanya wanafunzi waweze kupata data mbalimbimbali katika usomaji wao {EXTENSIVE READING} hivyo kupanuka kimawazo na kiakili, uhaba Wa computer kwa shule zenye tahasusi za computer, pia shuleni kumekua na uhaba Wa kamusi, dictionaries, na hata Atlas kwa ajiri ya kufundishia michoro ya ramani, sambamba na hilo kwenye Advanced secondary schools serikali imekua na tabia ya kutopeleka calculater kwa shule zenye tahasusu ya masomo ya hisabati, uhaba Wa vifaa vya maabara kwa tahasusi za sayansi nacho ni kikwazo kwa ufaulu Wa wanafunzi.
Ni kweli maafisa elimu wanaweza kuchangia kuinua elimu, lakini hii ni kwa asilimia chache sana kwani watu wanaokaa karibu sana na wanafunzi huwa ni walimu, hivyo walimu ndio watu Wa kuangaliwa kwa jicho la tatu ili wanafunzi wapate kuongoza kwenye taaluma kuliko kwenye michezo kama anavyodai RC Makonda.
Walimu wamevunjwa moyo {they be disappointed }, kwani baadhi wanaishi maisha magumu sana katika majumba mabovu, wananyimwa sitahiki zao kama kupanda madaraja na kuongezewa mishahara kila baada ya mwaka.
Hizi ndio changamoto zinazowakabili walimu wetu zinazowapelekea kuvunjwa moyo na serikali hadi kupelekea wao kuweka migomo baridi katika swala la ufundishaji, maana wamekua wakitishiwa kila iitwapo leo kufutwa kazi wanapokua wanaandamana kudai masilahi yao,
Kwakua wanauhitaji na kazi ndio maana wameamua kufanya mgomo baridi Wa kufundisha bila kujali kama mwanafunzi ameelewa au la! ndio sababu inayopelekea baadhi ya watoto Wa kileo wanamaliza darasa la saba bila kujua KUSOMA wala KUANDIKA.
Hii inatokana na Mwalimu kutojiumiza kichwa kwa mtoto Huyo, kwani anaona kama anafanya kazi ambayo mshahara wake unakua mdogo kuliko kazi anayoifanya {UNYONYWAJI}, hivyo kupelekea kutomsimamia mtoto ipasavyo ili aelewe kile anachokifundisha,
Mwanzoni Mwalimu alikua hawezi kufundisha bila kuacha zoezi darasani na kusahihisha,
Lakini sasa hivi kwakua walimu wame be disappointed na serikali, inawawia vigumu kutoa mazoezi ili kubaini yupi ameelewa na yupi hajaelewa hivyo kupelekea ufaulu hafifu Wa wanafunzi katika Mitihani yao ya taifa ya kumaliza elimu ya msingi na sekondari nchini.
Wito wangu kwa RC Makonda.
Kabla hajaanza kuwashughulikia maafisa elimu , ni bora akaishauri kwanza serikali kupeleka vifaa sitahiki mashuleni ili wanafunzi wapate kujifunza vyema, bila kusahau kuwalipa walimu sitahiki zao na madeni wanayoidai serikali ndipo aanze kula sahani moja na maafisa elimu ili waanze kusimamia ipasavyo swala la elimu bila kukutana na maswali yasiyojibika na vikwazo mbalimbali kutoka kwa walimu , vinginevyo hata kama RC Makonda atawalazimisha maafisa elimu wawawajibishe walimu ambao hawafundishi ipasavyo, hii itakua kama kutwanga maji kwenye kinu ambapo walimu hawataliafiki kamwe kwani ni mda mrefu wamekua wakidai sitahiki zao bila mafanikio,
MP Esrom Fubusa
(Mwanaharakati)
Mobile:0628998300
Email: kakafubusa87@gmail.com
No comments