TCRA yazitaka kampuni za simu kusitisha matangazo kwenye miito ya simu
Mamlaka ya mawasiliano nchini Tanzania TCRA imeziwataka wamiliki wa mitandao ya simu nchini kusitisha matangazo yanayosikika kabla ya muito wa simu pindi mteja anapopiga simu.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA,James Kilaba ambapo amesema kuwa matangazo hayo yamekuwa kero kwa watumiaji wa mitandao ya simu nchini.
Aidha Kilaba anazitaka kampuni za simu kusitisha matangazo pindi mtu anapopiga siomu kabla ya muito huku akisema matangazo hayo yamekuwa kero kwa watumiaji wa mitandao ya simu na hivyo kutoa wito kwa kampuni za simu zote kurudi katika utaratibu wa kawaida mtu anapopiga simu akutane na miito ya kawaida na si matangazo.
“Tunachoongelea ni kwamba kama mtu unapiga simu moja kwa moja ianze ringtone au yenyewe imeweka au mwenyewe umechagua lakini tunataka ianze kwenye ringtone ianze kuring kama hapatikani iseme ni busy tone moja kwa moja sio kwamba uanze utangulizi ukiisha huo ndio ije ringtone sasa hivi ndicho kinachotokea kwa baadhi ya makampuni ya simu,” alisema Kilaba.
No comments