Sakata la mimba mashuleni: Diamond Platnumz ‘ampa tano’ Rais Magufuli
Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amemuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli kwa kauli yake aliyoitoa mkoani Pwani wiki iliyopita kuwa Wanafunzi wa kike wanaopewa mimba mashuleni wasirudi kuendelea na masomo kwenye shule za Serikali.
Rais Magufuli na Diamond Platnumz
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Kigali jana jioni amesema hawezi kupingana na Rais Magufuli kwani mpaka kuchaguliwa na Watanzania ni ishara kuwa anakubalika kwa kila kitu anachokifanya.
“He is the president, so siwezi kubisha, mpaka alipochaguliwa kuwa rais, ina maana tumekubaliana na akili yake tumeona anafaa,” amesema Diamond.
Diamond Platnumz ambaye leo atatumbuiza mjini Goma nchini DR Congo kwenye mkutano wake na waandishi wa habari nchini Rwanda jana jioni ameongeza kwa kusema kuwa “siwezi kujua ni kwa sababu gani mpaka Magufuli amesema hivyo”
Diamond Platnumz na Vanessa Mdee ni moja ya Wasanii wanaotarajiwa kutumbuiza kwenye tamasha la Fiesta Rwanda ambalo litafanyika Julai 2 mwaka huu jijini Kigali, Bongo5 itakupatia Exclusive zote zitakazojiri kwenye tamasha hilo.
No comments