Polisi Watanda kwenye Viwanja vya Bunge , wakati Muswada wa Sheria ukijadiliwa
Polisi wakiwa katika magari yao, leo wameonekana wakirandaranda kwenye viwanja vya Bunge mjini hapa wakati wadau wakitoa maoni kuhusu muswada wa marekebisho wa sheria mbalimbali wa mwaka 2017.
Muswada huo unalenga katika kuboresha sheria zinazohusiana na rasilimali za Taifa.
Alipopigiwa simu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa amesema kuwa yupo kwenye kikao na kwamba apigiwe baadaye.
Wadau mbalimbali kwa siku nzima leo watatoa maoni yao kuhusu muswada huo ambao unatarajiwa kuwasilishwa bungeni ili kujadiliwa keshokutwa.
No comments