Maxime ataka kuinoa Taifa Stars
Nahodha wa zamani wa Taifa Stars, na Kocha mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Maxime amesema Stars inahitaji kocha ambaye ana uwezo wa kutambua wachezaji wenye vipaji, malengo na moyo wa kujituma ambao wataisaidia timu hiyo kusaka matokeo mazuri.
"Mimi nasema bado Stars haijapata kocha anayefaa kuinoa timu hiyo, kuna mambo mengi yanaendelea, lakini itafika wakati mtu sahihi atapewa jukumu hilo, ninaweza, umri wangu bado mdogo ninaamini itafika siku nitapewa mikoba na wataona uwezo wangu" alisema.
Maxime amesema anaamini ipo siku atapata nafasi ya kuifundisha timu hiyo na matokeo ya furaha ambayo yanaliliwa na Watanzania yatapatikana.
No comments