Breaking News

SERIKALI IMEIPA SIKU 24 KAMPUNI YA MOHAMED ENTERPRISES KUYARUDISHA MASHAMBA YA MKONGE KOROGWE

Serikali imeipa siku 24 kampuni ya Mohamed Enterprises kuyarudisha mashamba ya mkonge inayoyamiliki ya Mazinde Group yenye ukubwa wa hekta 9418 ambayo miongoni mwake hayajaendelezwa

Naibu waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi Angelina Mabula ametoa maagizo hayo baada ya kutembelea mashamba ya Mkonge yanayomilikiwa na kampuni hiyo wilayani Korogwe

Meneja wa mashamba hayo Imamu Sheketo ameahidi wataanza kuyaendeleza kwa sababu vifaa tayari wanavyo

Naibu waziri amewataka wataalamu kufika katika mashamba hayo na kuyataja ambayo hayajaendelezwa

Waziri pia amesema mashamba hayo yametumika kuchukua mikopo benki lakini mikopo hiyo haijatumika kuendeleza mashamba hayo

Mbunge wa Korogwe Prof. Maji Marefu amesema hatua hiyo itasaidia wananchi wa Korogwe ambao walikuwa wakilia kwa muda mrefu

No comments