Breaking News

MWILI WA MTOTO ALIESOMBWA NA MAJI WAPATIKANA

Hatimaye mtoto Samson Sanga aliyepotea baada ya kuzolewa na maji na kuzama kwenye bwawa la Nabwada katika manispaa ya Mtwara/Mikindani,kufuatia mvua kubwa iliyonyesha kwa siku mbili mfululizo katika mji wa Mtwara,amepatikana akiwa ameshakufa,kufuatia kazi kubwa ya kumtafuta iliyofanyika kwa zaidi ya saa 7, ikishirikisha wataalamu kadhaa wa kupiga mbizi majini.

Akizungumza baada ya mwili wa mtoto Samson kupatikana,mmoja wa wapiga mbizi hao Abati Mani amesema walifanikiwa kumwona mtoto huyo na kumwopoa maji akiwa anaelea,baada ya kumtafuta kwa kuzunguka bwawa hilo mara kadhaa,bila mafanikio.

Tukio la kuopolewa mwili wa mtoto Samson Sanga lilishuhudiwa na mkuu wa mkoa wa Mtwara Gelasius Byankanwa,kamanda wa polisi mkoani Mtwara Naibu Kamishna wa polisi Lucas Mkondya na mbunge wa Mtwara mjini Maftaha Nachuma,ambapo mkuu wa wilaya wa Mtwara Evod Mmanda amesema,ipo mipango ya kujenga mfereji wa kupeleka maji ya bwawa hilo la Nabwada yaende baharini,lakini changamoto kubwa,kuna watu waliojenga kuta na kusababisha maji yashindwe kwenda baharini.

Akizungumza na wananchi waliojitokeza kushuhudia,Mkuu wa mkoa wa Mtwara Glasius Byankanwa mbali na kuwapa pole familia na wakazi wote wa Mtwara kwa tukio hilo, ameagiza Manispaa ya Mtwara/Mikindani kuanza kuweka alama kuzunguka bwawa hilo, kuzuia watu kuendelea kujenga,na pia ameagiza waliojenga kutakwenye njia ya maji,kuta hizo zibomolewemara moja.

No comments