Breaking News

VIONGOZI NA WANACHAMA WA CHADEMA WANAOTAJWA KUTAKA KUKIHAMA CHAMA HICHO

Siasa za Tanzania  kama mchezo wa mpira wa miguu. Vyama  vinachuana katika kufanya usajili wa wanachama wapya kwa ajili ya mtifuano hapo 2020.

Siku za hivi karibuni tumeshuhudia baadhi ya wanasiasa kuhama vyama vyao na kuhamia vyama vingine.

Alianza aliekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini,Ndugu Lazaro Nyarandu ambapo alitangaza kujivua Ubunge na uanachama wa CCM na baadae kujiunga na CHADEMA.

Siku chache baadae,Prof. Kitila Mkumbo nae alitangaza kurudi CCM.

Juzi tumepata taarifa kuwa aliyekuwa mwenyekiti  wa BAVICHA,Ndugu PatrobasKatambi ,Mwanasheria Albert Msando  na wengine wamejiunga na CCM.

Pia aliyewahi kuwa  mbunge wa Kigoma Kaskazini kwa tiketi ya CHADEMA, David Kafulila ametangaza kujivua  uanachama wa CHADEMA.

Lakini  kuna tetesi kuwa kuna viongozi na wanachama wengine wa CHADEMA ambao wanahisiwa kutaka kukihama chama hicho . Hapa chini ni baadhi yao

1.Edward Lowassa-Lowassa anatajwa kutaka kurudi katika chama chake cha awali cha CCM ingawa mwenyewe amekanusha taarifa hizo

2.Vicent Mashinji-Huyu ni katibu mkuu wa CHADEMA, nae anatiliwa shaka kutaka kukikacha chama hicho lakini mwenyewe ameibuka na kukanusha uzushi huo

3.Malisa Gj-Ni kijana tegemezi katika harakati za chama.Kutokana na uswahiba wake na Albert msando na yeye anahisiwa wenda akafuata nyayo za swahiba wake Malisa nae amekanusha uzushi huo

4.Isaya Mwita-Huyu ni mstahiki meya wa jiji la Dar es salaam, nae anatajwa kwenye sakata la kutaka kujiondoa CHADEMA.Mwita baada ya kupata taarifa   hizo ameibuka na kuzikanusha na kusema hana mpango huo

5.Wema Sepetu na Mamayake-hawa waliondoka CCM wakati wa sekesekela madawa ya kulenya,lakinileo hii wanatajwa kutaka kurejea CCM. Wema sepetu amekanusha taarifa hizo.

Hao ni baadhi ya makada wa CHADEMA wanatajwa kutaka kukikacha chama hicho, lakini karibia wote baada ya kupata uzushi huo kwa wakati tofauti wameibuka na kukanusha uzushi huo kwa kusema hawana mpango huo.

No comments