Breaking News

KUNA UMUHIMU WA KILA MTU KUFANYA KAZI

 


Mchungaji Kiongozi wa kanisa la Mikocheni B Assemblies Of God, maarufu kama ‘Mlima wa Moto’ Getrude Lwakatare amesema ni muhimu kila mtu kufanya kazi kwa bidii ili kupunguza utegemezi.

Akizungumza na waandishi wa habari kanisa kwake, wakati wa uvunguzi wa kongamano la kuwainua wanawake kiuchumi mwaka 2017.

“Leo tuna kongamano maalum la wanawake na uchumi, lengo ni kufikia uchumi na viwanda mwaka 2025 na wanawake nao waweze kuwa na sehemu katika hili, kwahivyo tuna mafundisho mbalimbali ya kuwafundisha kina mama hasa kuwahizmiza kuna umuhimu wa kila mtu kufanya kazi.” alisema Mama Lwakatare.

Kongamano hilo liliandaliwa na kanisa la Mikocheni B Assemblies Of God jijini Dar es salaam ambapo Mama Lwakatare alisema kongamano hilo linalenga kumfanya mwanamke kuwa sehemu ya uchumi wa kati.


No comments