Breaking News

Polisi 200 wamwagwa kudhibiti mashabiki wa Chelsea, Roma leo

Mchezo wa Chelsea na Roma unatarajiwa kuwa na ushindani mkali ndani na nje ya uwanja kutokana na kila timu kuhitaji ushindi leo.

 Zaidi ya polisi 200 watakuwa na kibarua cha kuhakikisha usalama unaimarika nje na ndani ya uwanja kutokana na kuwapo viashiria vya vugugu tangu jana wakati timu hizo zilipokuwa zikiendelea na mazoezi.

Italia. Zaidi ya mashabiki wa Chelsea 2,000 wanatarajiwa kuishangilia timu yao itakayokuwa jijini Rome kumalizana na Roma kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya leo Jumanne.
Zaidi ya polisi 200 watakuwa na kibarua cha kuhakikisha usalama unaimarika nje na ndani ya uwanja kutokana na kuwapo viashiria vya vugugu tangu jana wakati timu hizo zilipokuwa zikiendelea na mazoezi.
Polisi nchini humo imetangaza kuimarisha usalama ambapo kikosi cha Chelsea kilifanya mazoezi yake jana Jumatatu.
Timu hizo zinaingia uwanjani baada ya mchezo uliopita uliofanyika Stamford Bridge kuisha kwa sare ya mabao 3-3.
Kuna tetesi kwamba mashabiki wa klabu pinzani ya Lazio huenda wakaungana na wale wa Chelsea kuwavuruga mashabiki wa Roma kuelekea kwenye mechi.
Awali, mashabiki wa Roma walifanya vurugu mwanzoni mwa mwezi huu wakiwa London jambo ambalo linatajwa huenda nao wapenzi wa Chelsea wakarudisha kisasi.

No comments