Breaking News

Kipa Yanga apitia ya akina Barthez


Kakolanya alishuhudia namna ambavyo Barthez na Dida walivyowekana benchi ambapo ilikuwa mmoja akianza kucheza mwingine anasahaulika, kama inavyotokea sasa na kaweka wazi kwamba siku atakapokaa langoni, basi kocha atakubali ufundi wake

KIVULI cha makipa walioondoka Yanga, Deo Munishi ‘Dida’ na Ally Mustapha ‘Barthez’, ni kama kimehamia kwa walioziba nafasi zao ambao ni Beno Kakolanya na Youthe Rostand ambaye nyota yake kwa sasa inang’aa.

Kakolanya alishuhudia namna ambavyo Barthez na Dida walivyowekana benchi ambapo ilikuwa mmoja akianza kucheza mwingine anasahaulika, kama inavyotokea sasa na kaweka wazi kwamba siku atakapokaa langoni, basi kocha atakubali ufundi wake.

“Nimesumbuliwa na majeraha kwa muda mrefu, lazima kocha atalazimika kumtumia yule ambaye yupo fiti, ndiyo maana nasema hadi atakaponipanga ndipo atajua nina ubora kiasi gani, lakini kwa sasa si rahisi,”alisema

Hali hiyo alisema siyo ngeni kwake kwani alipata uzoefu kwa akina Barthez na Dida.

Hana wasiwasi na nafasi yake kama alivyoeleza kuwa yupo makini kuangalia ubora na udhaifu wa kipa mwenzake, jambo analoamini litampa hatua nyingine, akija kucheza atakuwa na jipya.


No comments