KATIBU MWENEZI CCM AHAMIA CHADEMA
Amehamia chama hicho akieleza wakati wa ukombozi umefika
Aliyekuwa Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Nyasa, Staniford Emmanuel amehamia Chadema kwa maelezo kuwa wakati wa ukombozi umefika.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi kadi hiyo kwa viongozi wa Chadema, Emmanuel amesema wakati wa ukombozi umefika hivyo hana budi kuhama CCM ili aweze kutendea haki nchi yake.
“Kuna wanaCCM wenzangu bado hawajafanya maamuzi kama niliyoyafanya mimi kujiondoa na kuhamia chama cha ukombozi ambacho mimi nimekiona ni Chadema,”amesema Emmanuel.
No comments