Breaking News

NAFASI YA SIMBA LEO KUONGOZA #VPL ENDAPO ITASHINDA

 

Endapo Simba itashinda mchezo wake wa ligi kuu Tanzania bara leo Jumapili dhidi ya Stand United, itafikisha pointi 11 na kuongoza ligi kutokana na wastani wa magoli.

Kwa sasa Simba ipo nafasi ya sita ikiwa na pointi nane baada ya kucheza mechi nne, mchezo mmoja nyuma ya vinara wa ligi Mtibwa Sugar na Azam ambazo kwa pamoja zina pointi 11 lakini Mtibwa ndio ipo kwenye nafasi ya kwanza kwenye msimamo kutokana na tofauti ya magoli.

Simba inacheza leo mechi yake ya tano ya ligi ugenini dhidi ya Stand United, iwapo itashinda itafikisha pointi 11 na kuitoa Mtibwa kwenye uongozi wa ligi kwa sababu ‘Wekundu wa Msimbazi’ wana idadi nzuri ya wastani wa magoli.

Rekodi inaibeba Simba katika mechi ambazo imecheza dhidi ya Stand United, katika michezo sita iliyopita Simba imeshinda mara nne, Stand imeshinda mara mmoja na mchezo mmoja timu hizo zilitoka sare.

12/05/2017 Simba 2-1 Stand United

02/11/2016 Stand United 0-1Simba

13/02/2016 Stand United 1-2Simba

30/09/2015 Simba 1-0 Stand United

21/02/2015 Stand United 1-0 Simba

04/10/2014 Simba 1-1 Stand United

Hadi sasa kila timu imeshacheza mechi nne za ligi msimu huu, Simba imeshinda michezo miwili na kutoka sare mara mbili wakati Stand United yenyewe imeshinda mechi moja tu katika michezo minne waliyocheza tangu kuanza kwa msimu.

Stand United msimu huu

Mtibwa Sugar 1-0 Stand United

Lipuli 1-0 Stand United

Stand United 0-Singida

Stand United 2-1 Mbeya City

Simba msimu huu

Simba 7-0 Ruvu Shooting

Azam 0-0 Simba

Simba 3-0 Mwadui

Mbao 2-2 Simba

Simba bado haijashinda ugenini msimu huu, imecheza mara mbili nje ya uwanja wa Uhuru na kuambulia sare (Azam 0-0 Simba, Mbao 2-2 Simba). Stand imeshinda mechi moja tu kati ya nne ilizocheza, imeshinda nyumbani (Stand United 2-1 Mbeya City) huku ikiwa imepoteza mechi mbili ilizocheza nje ya Shinyanga (Mtibwa Sugar 1-0 Stand, Lipuli 1-0 Stand).


No comments