Wenger aanza kukata tamaa kwa Sanchez
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger, amesema hakuna maelewano yoyote kwenye mkataba mpya kati ya washika bunduki hao na mpachika mabao wake mahiri Alexis Sanchez.
Sanchez mwenye miaka 28, mkataba wake upo chini ya miezi 12, kuendelea kuitumikia klabu hiyo.
“Huyu ni mchezaji ambaye yupo kwenye mwaka wa mwisho wa mkataba wake,” alisema Wenger, na kuongeza kuwa “hatuna muendelezo juu ya jambo hilo”
Bosi huyo wa The Gunners, anaonekana kama ameinua mikono juu kuhusu mchezaji huyo ambaye kiangazi kijacho huenda akaondoka pasi na gharama yoyote.
“Wacha tusiwe na makosa, siyo jambo lenye kuvutia haswa upande wa masuala ya kifedha na inahitaji kujitoa mhanga kwa kiasi fulani,” aliongeza Mfaransa huyo.
Wenger alikuwa na matumaini kwamba angeweza kumkaribisha nyota huyo kwenye mapambano hasa kwenye mechi iliyo mbele yao ya Ligi Kuu ya England dhidi Liverpool mnamo Agosti 27.
No comments