Breaking News

MEYA WA UBUNGO AWAONDOA KIULAINI WAMACHINGA WALIOKUWA WANAFANYA BIASHARA BARABARANI YA UBUNGO.


Mstahiki Meya wa halmashauri ya manispaa ya Ubungo, amefanya mkutano wa hadhara Ubungo Mataa na kuweza kukubaliana na wamachinga hao kupisha ujenzi wa 'Flyover' katika maeneo hayo na kuwataka kwenda kufanya biashara zao sehemu nyingine.

Boniface Jacob aliongozana na Mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya Ubungo Bw.John Kayombo pamoja na maofisa kutoka ofisi za TANROANDS, Jeshi la Polisi, Wizara ya Ujenzi pamoja na Mkandarasi wa 'Flyover' Ubungo CCI- CCE

Meya Boniface Jacob amesema kuwa lengo lao kuu lilikuwa kuwaondoa wafanyabiashara hao wadogo pasipokuwa na vurugu zozote na amewataka watu wengine kujifunza kutoka katika halmashauri hiyo jinsi ilivyoweza kukubaliana na wamachinga hao kuwaondoka katika maeneo hayo kupisha ujenzi huo pasipokutumia nguvu ya vyombo vya ulinzi na usalama.

Aidha amewaruhusu wamachinga kwenda kupanga biashara zao popote pale barabarani nje ya eneo la mradi, watakapo ona inafaa bila ya kubughuziwa na mtu yeyote, kufuatisha kauli ya Mheshimiwa Rais Magufuli kuwa wamachinga wasisumbuliwe, na kwa Wale watakao taka kurejea kituo cha Mawasiliano, Manispaa ya Ubungo imeandaa utaratibu mzuri wa Kuponi maalumu kwa wamachinga wa Ubungo.

No comments