Breaking News

Mbunge mwingine Chadema ahojiwa na Polisi

Mbunge wa Viti Maalum (Chadema) Kunti Majala

Mbunge huyo aliitwa na polisi kuhojiwa baada ya kupokea malalamiko kuwa alikuwa akiitukana Serikali na kutumia lugha chafu katika shughuli zake za kisiasa kwenye jimbo hilo.
Viongozi tisa akiwamo Katibu Mkuu wa Chadema, Vincent Mashinji walikamatwa juzi  na Polisi wilayani Nyasa kwa kufanya kusanyiko lisilo halali.

Dodoma.  Mbunge wa Viti Maalum (Chadema) Kunti Majala alishikiliwa na polisi kwa zaidi ya saa tatu akidaiwa kufanya kusanyiko lisilo halali katika kijiji cha Mapango, kata ya Chandama wilaya ya Chemba mkoani Dodoma jana jioni.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumanne, Julai 18, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa amesema mbunge huyo aliitwa na polisi kuhojiwa baada ya kupokea malalamiko kuwa alikuwa akiitukana Serikali na kutumia lugha chafu katika shughuli zake za kisiasa kwenye jimbo hilo.

Pia amesema mbunge huyo alikuwa akifanya mkutano wa hadhara bila kuwa na kibali cha polisi.

Hata hivyo, Kunti amesema kuwa aliruhusiwa kufanya mkutano huo na Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Chemba kwa njia ya simu.

Hata hivyo jana alipomaliza kuhojiwa, polisi walitoa barua ya kukataza mikutano yake ya hadhara aliyokuwa aifanye jimboni humo kuanzia jana hadi Julai 20.

No comments