Akamatwa na meno ya Tembo yenye thamani ya Sh 33 milioni
Kamanda wa polisi mkoani Morogoro, Ulrich Matei akizungumza leo Jumatatu na waandishi wa habari amesema mtuhumiwa alikamatwa nyumbani kwake maeneo ya Kata ya Mlali Wilaya ya Mvomero na askari waliokuwa doria.
Jeshi la polisi mkoani Morogoro linamshikilia Kimosa Kibona(43) Mkazi wa Tarafa ya Mlali kwa tuhuma za kukutwa na pembe mbili za ndovu zenye thamani zaidi ya Sh 33 milioni.
Kamanda wa polisi mkoani Morogoro, Ulrich Matei akizungumza leo Jumatatu na waandishi wa habari amesema mtuhumiwa alikamatwa nyumbani kwake maeneo ya Kata ya Mlali Wilaya ya Mvomero na askari waliokuwa doria.
Matei amesema kukamtwa kwa mtuhumiwa huyo ni baada ya polisi kupokea taarifa za kiintelijensia ndipo walipofika nyumbani kwake na kumpekua na kukutwa akiwa na pembe hizo mbili zikiwa zimehifadhiwa katika salfeti pamoja na pilipili mbili sina ya SunLG.
No comments