WANAFUNZI WALIONUSURIKA KIFO AJALI YA GARI ARUSHA WAFANYIWA UPASUAJI MAREKANI
Watoto watatu wa shule ya msingi ya Lucky Vicent walionusurika katika ajali ya basi, wamefanyiwa upasuaji na sasa wapo wodini wakiendelea na mazoeazi, ila Doreen, jana alipewa MAPUMZIKO maalumu akiwa anaandaliwa tayari kwa UPASUAJI wa uti wa mgongo 'spine' unaofanyika leo.
Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu aliyeshiriki katika kuwasafirisha watoto hao, ameandika katika ukurasa wake wa facebook akisema watoto hao kwa sasa wamewekwa kwenye vyumba vya peke yao.
Upasuaji huo umefanyika katika Hospitali ya Mercy, Sioux City, Marekani.
Amefafanua upasuaji waliofanyiwa na kusema mtoto Saidia alifanyiwa upasuaji wa mfupa wa kulia wa nyonga, mkono wa kulia na kuwekewa ngao kwenye shingo atakayotakiwa kukaa nayo kwa wiki sita.
“Kwa upande wa mtoto Wilson, yeye amefanyiwa upasuaji wa nyonga ya kulia, kiwiko cha kulia kilichokuwa kimevunjika mara tatu na kiwiko cha kushoto,” amesema
Amesema Doreen yeye amefanyiwa upasuaji wa nyonga, taya katika upasuaji uliochukua saa nne. Leo Doreen atafanyiwa upasuaji wa uti wa mgongo.
Advertisement
Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255742 532203
No comments