Antonio Conte amtimua Diego Costa Chelsea.
Kumbe ule uliotajwa kama ugomvi kati ya Diego Costa na kocha wake Antonio Conte ambao ulitokea katika dirisha lililopita la usajili haujaisha, kama unakumbuka kulikuwa na tetesi kwamba Costa alilazimisha kuuzwa China jambo ambalo lilimkera Conte na kuamua kumuacha katika mchezo mmoja wa ligi.
Baadae mambo yalionekana kuwa sawa na Conte akasisitiza hakuna tatizo kati yake na Costa na kwamba mshambuliaji huyo anaipenda Chelsea na hana mpango wa kuondoka na kuanzia hapo taarifa za msuguano kati ya hao wawili zikazimwa na Costa akaendelea kucheza Chelsea na kwa kiwango cha juu kabisa.
Takribani mwezi sasa umepita tangu Chelsea watwae ubingwa na Diego Costa ameibuka na kusema kwamba kocha Antonio Conte amemtumia ujumbe na kumuambia “haupo kwenye mipango yangu”, Costa aliyasema hayo kwa kinywa chake wakati wa mchezo wa kirafiki kati ya Hispania na Colombia.
“Kama hawanihitaji nitaanza kutafuta timu mpya, kwenda Atletico itakuwa jambo jema kwangu lakini itabidi nifikirie upya, kombe la dunia limekaribia lazima niende sehemu ambayo nitapata muda mrefu wa kucheza siwezi kaa sehemu ambayo nitapewa miezi mitatu au minne tu kucheza” alisema Costa.
Tayari inaonekana Conte amesahau msaada mkubwa wa Costa kwani mabao 20 na assist 3 alizotoa msimu huu zilichagiza kwa kiasi kikubwa ubingwa wa Chelsea lakini Conte hana mpango naye tena na tayari ameanza kumtafutia mtu wa kukaa nafasi yake huku Romelu Lukaku akitajwa kuwa mbadala wa Costa.
No comments