Breaking News

Mlinzi ahukumiwa miaka miwili jela kwa wizi wa gari la Serikali

Mlaponi ambaye ni mkazi wa Buza, amehukumuwa kifungo hicho leo(Alhamisi) katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la uzembe akiwa mlinzi.

Dar es Salaam.  Mlinzi wa Kampuni ya Ulinzi ya Security Guard, Charles Mlaponi (54) amehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela baada ya kupatikana na hatia ya wizi wa gari la Serikali, mali ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Mlaponi ambaye ni mkazi wa Buza, amehukumuwa kifungo hicho leo(Alhamisi) katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la uzembe akiwa mlinzi.

Pia, mahakama hiyo, imewaachia huru washtakiwa wawili katika kesi hiyo ambao ni Emmanuel Remmy (37) maarufu Mosha ambaye ni dereva wa gari lililoibiwa na George Mwaipungu (39) ambaye ni mfanyabiashara.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mfawidhi, Ritha Tarimo aliiambia mahakama kuwa ameridhishwa na ushahidi uliotolewa na mashahidi wanne dhidi ya mshtakiwa huyo na hivyo kumtia hatiani kama alivyoshtakiwa. 

“Mlaponi utatumikia kifungo cha miaka mwili jela ili iwe fundisho kwa walinzi wengine ambao ni wazembe katika maeneo yao ya lindo na nafasi ya kukata rufaa iko wazi kama hujaridhishwa na hukumu hii,” alisema Hakimu Tarimo. ,

Akipitia baadhi ya ushahidi uliotolewa mahakamani hapo, Hakimu Tarimo alisema Mlaponi alikabidhiwa gari hilo eneo la Tabata Relini na mshtakiwa wa pili katika kesi hiyo ambaye ni dereva wa gari hilo ili alilinde.

No comments