Breaking News

Mbuge Kaunje Asema Serikali Haipendelei na Haina Ubaguzi katika Kuhudumia Wananchi

Na. Ahmad Mmow, 
Lindi. MBUNGE wa jimbo la Lindi mjini, Hassan Kaunje, amewataka wananchi kuachana na fikra potofu kwamba serikali inaupendeleo na ubaguzi katika kutoa huduma kwa wananchi. Kaunje aliyasema hayo baada ya kukabidhi msaada wa mfuko 40 ya saruji itakayo tumika kujengea uzio katika shule ya msingi ya Rahaleo iliyopo katika manispaa na wilaya ya Lindi. Kaunje ambae pia alikabidhi mifuko 30 ya saruji katika kata ya Mwenge itakayotumika kujengea ofisi ya kata hiyo, alisema hakuna ukweli wowote uaozungumzwa na baadhi ya watu wenye lengo baya dhidi ya serikali kwa wananchi. 

Kwamba wananchi wa eneo fulani hawathaminiwi na serikali kuliko wenzao wa eneo jingine. Alisema dhana hiyo haina ukweli wowote, hivyo hawana budi kuibua miradi ya maendeleo na kuanza kutekeleza badala ya kusubiri serikali ambayo I anajukumu mengi. Alibainisha kwamba maeneo yanayotajwa kupendelewa niyale ambayo wananchi wake wanaonesha kuwa  na kiu ya maendeleo kwa kuanzisha na kuibua miradi ya maendeleo kwa kutumia nguvu zao wenyewe bila kusubiri serikali. 

Ndipo serikali hulazimika kwenda kusaidia. "Hizo ni propaganda za wanasiasa zenye malengo ya kisiasa, bali ukweli ni huo. Hakuna ubaguzi wala upendeleo wowote," alisema Kaunje. Mbunge huyo alitolea mfano taarifa iliyokuwa imeripotiwa katika baadhi ya vyombo vya habari wakati wa mauzo ya zao la korosho msimu uliopita, kwamba baadhi ya wakulima baada ya kupata fedha walinywesha mbuzi soda . 

 Alisema iwapo  habari hiyo ilikuwa ya kweli, inatosha kuwa ni ushahidi unaodhihirisha kwamba wananchi wa mikoa hii (Lindi na Mtwara) wanashindwa kutambua matumizi sahihi ya fedha kuliko maeneo mengine. "Ninajambo la aibu nasio la kujivunia mnatuweka katika wakati mgumu wawakilishi wenu, mbuzi tunawanywesha soda, lakini mikoa hii mawili imeburuza mkia kwenye viwango vya ufaulu kwa shule za msingi na sekondari, kama sio aibu tuite nini," alihoji kwa huzuni Kaunje. 

 Aliweka wazi kwamba mambo kama hayo ni miongoni mwa sababu zinachangia tofauti za maendeleo baina ya eneo moja na jingine. Kwa madai kwamba kiasi hicho cha fedha wangepata wakulima wa Kanda nyingine wangetumia kwa shuguli za maendeleo. Ikiwamo kuchangia ujenzi wa zahanati, shule, nyumba za walimu na visima vya maji. Hivyo wangeongeza tofauti ya muonekano wa kimaendeleo. 

 "Sasa wanasiasa wanatumia udhaifu wetu kutulaghai ili wanufaike kisiasa, kwasababu mkiangalia tofauti mnaona kama kweli. Lakini hamjiulizi nikwanini, badala yake mnakubaliana nao na kuamini mnabaguliwa na hampendwi na serikali," alisema Kaunje. Kwa upande wake mwalimu wa taaluma wa shule hiyo, Hadija Singililo alisema miongoni mwa changamoto inayoikabili shule hiyo ni idadi ndogo ya walimu. Kwani pamoja na shule hiyo kuwa na wanafunzi takribani 800, lakini walimu waliopo ni 12 tu.

No comments