Chadema Walaani Tamko la Mwinyi Lakutaka Rais Magufuli Aongezewe Muda wa Utawala
Chadema imelaani vikali kauli ya Rais wa awamu ya pili, Ally Hassan Mwinyi aliyesema kuwa kama siyo matakwa ya Katiba ya nchi, uongozi wa Rais John Magufuli ulipaswa kuendelea kuwapo miaka yote.
Kiongozi huyo wa awamu ya pili ambaye alikuwa akizungumza kwenye swala ya Eid El Fitri alidai pia laiti ingelikuwa Katiba iliyopo haikufupisha muda wa uongozi wa urais, amengemshauri Rais Magufuli awe Rais wa Tanzania wa siku zote.
Akizungumzia kauli hiyo katika makao makuu ya Chadema yaliyopo Kinondoni, jana (Alhamisi) Katibu Mkuu wa Baraza la Wazee, Roderick Lutembeka amesema matamshi hayo yanapaswa kukemewa kwa vile yanaashiria kulipeleka Taifa kuandaa viongozi watakopuuza Katiba ya nchi.
“Sisi wazee wa Chadema kwa kutambua madhara ya kauli kama hizi tumeamua tusikae kimya kwani kauli hiyo inakiuka Katiba ya nchi inayoweza kulitumbukiza Taifa katika machafuko kama ambavyo imetokea kwa nchi jirani zilizopuuza uvunjifu wa katiba,” amesema.
Amewataka Watanzania kwa ujumla kujitokeza na kupinga kauli za namna hiyo ambazo alisema zinajaribu kuwaandaa wananchi kisaikolojia ili kuwa na viongozi watakaopindisha Katiba katika siku za baadaye
No comments