CCM Walaani Matamshi ya Lowassa......Waitaka Serikali Imchukulie Hatua
Chama cha Mapinduzi CCM kimelaani kauli za kichochezi na zakidini zilizofanywa na mmoja kati ya mwanasiasa nchini, zenye lengo la kuwafitinisha watanzania.
Katibu wa itikadi na uenezi wa chama cha mapinduzi CCM ndugu Humphrey Polepole amebainisha hayo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, huku akiiomba serikali ikithibitika mtu amekosea serikali isiwe na ajizi kuchukua hatua kwa aina ya mtu huyo.
Siku ya Jumanne na leo Alhamisi, aliyekuwa Mgombea Urais kwa Tiketi ya Chadema, Edward Lowassa amehojiwa na Jeshi la Polisi kwa kilichodaiwa kuwa ni maneno ya kichochezi aliyoyatoa kwa Waumini wa Dini ya Kiislamu wakati alipohudhuria Futari iliyokuwa imeandaliwa na Mbunge Waitara.
Katika futari hiyo, Lowassa anadaiwa kutoa maneno ya uchochezi kuhusu masheikh wa Taasisi ya Uamsho wanaoshikiliwa na magereza akidai kwamba utaratibu wa kisheria ufanyike ili kuwaachia huru masheikh hao.
Katika hatua nyingine, Polepole amesema kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinaunga Mkono Kauli ya Rais Magufuli ya kutorudi masomoni kwa wanafunzi waliopata ujauzito wakiwa shule kwenye mfumo rasmi wa Elimu.
Polepole amesema kuwa wanafunzi waliopata ujauzito hawataweza kurudi shuleni kwenye mfumo rasmi isipokuwa kwenye Mfumo wa elimu ya watu wazima.
No comments